Mkuu wa Mkoa wa Njombe amewatahadhalisha wananchi kutunza mazao ya chakula.
Ikiwa bei ya mazao ya chakula kama Mahindi yakiendele kupanda mwaka hadi mwaka, Mkuu wa Mkoa huo Captain Mstaafu Assery Msangi amwewatahadharisha wananchi wa Wanging’ombe na Njombe kwa ujumla kutouza mazao yote ya chakula.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kila Familia inatakiwa kutunza chakula cha kutosha ili Familia hizo zisipate adha ya njaa. Alisema kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa ataona aibu kuomba chakula cha Msaada kwa ajili ya Wananchi wa Njombe wakati Mkoa huo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na miongoni mwa mikao inayotegemewa kwa kuzalisha chakula nchini Tanzania.
Wakati Mkuu wa Mkoa huyo akitoa angalizo kwa wananchi wa Njombe, Wakala wa ghala la kuhifadhia chakula la Taifa Bwana Ibrahimu Saidi Nyangasa alisema kuwa Serikali imeweka vituo zaidi ya vinne vya kununulia Mahindi katika Mkoa wa Njombe Bwana Nyangasa alisema kuwa vituo hivyo vipo Makambako, Igwachanya, Shauri Moyo, Mawengi na Ludewa, vilevile alisema bei ya ya kilo moja ya mahindi ni kati ya shilingi mia tatu themanini (380) hadi mia nne (400).
Bwana Nyangasa alimuunga Mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa kuwataka Wananchi kuuza Mahindi ya ziada baada ya kutoa yale yanayowatosha kwa chakula.
Captain Msangi aliyasema hayo Jana katika Kata ya Igwachanya alipokuwa anahutubia wananchi wa Kata ya Igwachanya katika Wilaya Mpya ya Wanging’ombe.
No comments:
Post a Comment