Wednesday, November 28, 2012

KIFO CHA MSANII SHAROBARO.



Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la Chumba cha Kuhifadhia Maiti cha Hospitali ya Teule Muheza kwa ajili ya kushuhudia mwili wa msaniii Sharo Millionea aliyekufa katika ajali ya gari wakati akitoka Dar es Salaam kwenda Lusanga, Muheza mkoani Tanga, ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Kijiji cha Songa Kibaoni .
Wakazi wa wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya Chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza, kusubiri kushuhudia mwili wa Sharo Millionea, aliyefariki kwa

Tuesday, November 27, 2012

RC- AZITAKA HALIMASHAURI KUBUNI MBINU MBALIMBALI ZA KUONGEZA MAPATO.

Ikiwa kwa mara ya Kwanza kwa Mkoa wa Njombe kufanya  kikao cha kamati ya Ushauri  wa Mkoa  (RCC) toka  uwanze rasmi tarehe 2 Machi 2012,Mkuu wa Mkoa huo Capten (MST) Aseri Msangi  amezitaka Halmashauri za zinazounda mkoa wa Njombe kubuni miradi inayoweza kuwaingia kipato cha  kuwezesha  Halmashauri kujiendesha bila kutegemea  fedha toka Serikali kuu.
Msangi,alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Kyando kwenye kikao cha Ushauri wa Mkoa ambapo yeye ni Mwenyekiti,” Nashangaa kuona Halmashauri  zinatoa sababu ya kuchelewa kupata fedha toka Serikali kuu,wakati Halmashuri hizo zinashindwa kuimalisha mapato yao ya ndani’’,alizitaka kubuni miradi kama vile Ujenzi wa Nyumba za Kupangisha na Kufuga nyuki.
Alisema kuwa  Halmashauri zinauzo wa kukopa fedha kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha kwa kutekeleza miradi hiyo ambayo baadaye itaingizia Halmashauri fedha za kutosha za kujiendesha na kuendeleza Miradi ya maendeleo katika Mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Halmashuri zinauwezo wa kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki,mradi ambao hauwitaji Mbolea wala pembejeo ni mradi ambao unauwezo wa kuingizia fedha nyingi kwenye Halmashauri na mkoa kwa ujumla.
Mkoa wa Njombe umendwa na wilaya ya Njombe,Makete ,Wanging’ombe  na Ludewa wilaya zote hizo ni maarufu kwa kilimo cha Viazi mviringo,Mahindi na mazao ya misitu Kama Mbao, kwa bagdeti ya mwaka 2012/2013 ilikadiliwa kukusanya zaidi ya shilingi billion

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MAZAO YA CHAKULA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe amewatahadhalisha wananchi kutunza mazao ya chakula.
Ikiwa bei ya mazao ya chakula kama Mahindi yakiendele kupanda mwaka hadi mwaka, Mkuu wa Mkoa huo Captain Mstaafu Assery Msangi amwewatahadharisha wananchi wa Wanging’ombe na Njombe kwa ujumla kutouza mazao yote ya chakula.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kila Familia inatakiwa kutunza chakula cha kutosha ili Familia hizo zisipate adha ya njaa. Alisema kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa ataona aibu kuomba chakula cha Msaada kwa ajili ya Wananchi wa Njombe wakati Mkoa huo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na miongoni mwa mikao inayotegemewa kwa kuzalisha chakula nchini Tanzania.
Wakati Mkuu wa Mkoa huyo akitoa angalizo kwa wananchi wa Njombe, Wakala wa ghala la kuhifadhia chakula la Taifa Bwana Ibrahimu Saidi Nyangasa alisema kuwa Serikali imeweka vituo zaidi ya vinne vya kununulia Mahindi katika Mkoa wa Njombe Bwana Nyangasa alisema kuwa vituo hivyo vipo  Makambako, Igwachanya, Shauri Moyo, Mawengi na Ludewa, vilevile alisema bei ya ya kilo moja ya mahindi ni kati ya shilingi mia tatu themanini (380) hadi mia nne (400).
Bwana Nyangasa alimuunga Mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa kuwataka Wananchi kuuza Mahindi ya ziada baada ya kutoa yale yanayowatosha kwa chakula.
Captain Msangi aliyasema hayo Jana katika Kata ya Igwachanya alipokuwa anahutubia wananchi wa Kata ya Igwachanya katika Wilaya Mpya ya Wanging’ombe.







MKUU WA MKOA WA NJOMBE AIMIZA KILIMO CHA MATUNDA

Mkuu wa Mkoa Njombe Captain Mstaafu Assery Msangi amewataka Wananchi wa Njombe kujikita kwenye Kilimo cha Miti ya Matunda kama vile Maparachichi.
Alisema ili kuinua kipato cha mtu binafsi na familia, Mikoa na nchi kwa ujumla, kila Mwananchi anapaswa kulima zaidi ya Ekari moja ya Miti ya Matunda. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kuipa faida familia kwa kuongeza kipato.
Msangi aliyasema nayo jana alipokuwa anafanya ziara katika Kijiji cha Mdandu Kata ya Igwachanya Wilaya ya Wanging’ombe.
Katika ziara hiyo aliweza kutembelea shamba la Miti ya Matunda ya Bwana Dariko Ngota (42) ambaye amelima zaidi ya Ekari moja ya Miti ya Matunda aina ya Maparachichi.
Mkuu huyo wa Mkoa pia aliweza kutembelea Vitalu vya Miche ya Matunda aina ya Maparachichi ambayo inamilikiwa na Kikundi cha Mdandu.
Maparachichi yanayolimwa katika Mkoa wa Njombe ni aina ya Hass na x- Ikula na soko kuu la matunda hayo ni Mikoa ya Mbeya na Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Assery Msangi aliyavaa Miwani akikagua Shamba la Matunda aina ya Maparachichi katika kijiji cha Mdandu katika Wilaya ya Wanging’ombe.

KILIMO CHA CHAI CHAINUA UCHUMI WA MKOA WA NJOMBE


Moja ya mashamba ya chai yaliyoko Mkoa wa Njombe

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AHAMASISHA KILIMO CHA CHAI



Watu wa kada mbalimbali walijitokeza kwenye siku ya Utalii iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Turbo Mkoani Njombe,katika maadhimisho hayo yaliyofanyika mara ya kwanza toka Mkoa wa Njombe utangazwe kuwa Mkoa mwaka 2011.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Capt (MST) Aseri Msangi aliye wakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba.
Sarah Dumba alisema kua Mkoa mpya wa Njombe unavivutio vingi ambavyo vinaweza kutangazwa na kuongeza ajira kwa vijana  wa Njombe na kuongeza Kipato kwa wananchi wa Njombe na Tanzania kwa Ujumla.
Mkuu huyo wa wilaya alivitaja baadhi ya vivutio ambavyo vipo Mkoani Njombe pamoja na Msitu wa Asili wa Nyumbanitu ambao unavivutio vingi kama vile Kuku,Nyoka na sehemu ya Matambiko, Maporoko ya Mto Ruhuji,  Mamaki wa Mapamgo Mto Hagafilo Maeneo mengine yenye vivutio nikama chemichemi ya majimoto(Mbega), mapango ya wapiganaji wa vita vya majimaji (Utengule), Mafuvu ya watuwa kale(Nyikamtwe).  
Aliongeza kuwa Mkoa wa Njombe ,wananchi na wanahabari kwa ujumla wanatakiwa kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii amabavyo vipo mkoani humo ilikuweza kutambulika kitaifa na kimataifa,hii itasidia kuleta watalii mbalimbali kutoka ndani ya nchi na nnje ya nchi,na kuwomba watu mbalimbali kuwekeza kwenye sekta ya Utalii katika Mkoa huo.
Katika maadhimisho hayo bidhaa mbalimbali za kiasili ziliweza kuonyeshwa kwa wananchi ,bidhaa kama ,Mikeka, Vikapu,Viti na Vyungu,bidhaa zote hizo zilitengenezwa kwa vitu vya asili na wananchi wengi walijitokeza kununua bidhaa hizo.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi.Baruani Mgeni aliwomba wananchi mbalimbali kupigia kura vivutio vya Tanzania ili viingie kwenye maajabu saba ya Dunia,alivitaja vivutio hivyo ni Mlima Kilimanjaro,Serengeti na Ngorogoro ,pia alisema kuwa kwasasa Njombe ni mkoa ambao unajitegemea na utakuwa unafanya maonyesho ya utalii kila mwaka kama mikoa mingine inavyofanya.